Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, leo Mei 15, 2023 amewasili wilayani Bukombe mkoani wa Geita kwa ziara ya siku moja.
Akiwa wilayani Bukombe, Chongolo amezindua majengo mbalimbali ya Chama Cha Mapinduzi ukiwemo ukumbi wa mikutano, nyumba ya kupumzika wageni na mgahawa.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu huyo wa CCM amefuatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni, Issa Ussi Gavu.