Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake mkoani Pwani, baada kuhitimisha mbio hizo mkoani Morogoro.
Akipokea Mwenge huo mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amesema ukiwa Pwani, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika halmashuri tisa na kupitia miradi 99 yenye thamani ya shilingi Trilioni 4.4.
Amesema kati ya miradi hiyo, tisa itafunguliwa, 15 itazinduliwa, 20 itawekewa mawe mawe ya msingi na 55 itakaguliwa.