Arsenal imepoteza matumaini ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu baada ya kukubali kipigo cha magoli 3-0 kutoka kwa Brighton & Hove Albion.
Kufuatia kipigo hicho, Arsenal sasa inabaki nafasi ya pili ya msimamo wa ligi ikiwa na alama 81 baada ya kucheza mechi 36, huku Manchester City wanaopewa nafasi ya kushinda taji hilo wakiwa nafasi ya kwanza baada ya kujikusanyia alama 85 katika michezo 35.
Kwa msimamoa huo, Man City sasa inahitaji alama tatu kuwa bingwa kwani itafikisha alama 88 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
Arsenal itegemee muujiza au ndio imeumaliza mwendo?