Serikali yagharamia safari ya mashabiki 55 wa Yanga Afrika Kusini

0
236

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesaidia kugharamia usafiri wa mashabiki 55 wa timu ya Yanga kwenda Afrika Kusini katika mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Saidi Yakubu ikiwa ni hatua ya kuiunga mkono timu ya Yanga ambayo inatarajia kucheza mchezo wa pili dhidi ya Marumo Gallants Mei 17, 2023 kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng uliopo mji wa Rustenburg nchini humo.

Katibu Mkuu ameongeza kuwa “Katika mechi hizi, lolote linaweza kutokea lakini Serikali pamoja na Yanga kupitia idara tofauti tumejipanga vizuri, Waziri Pindi Chana anatoa salamu nyingi, pongezi na kuwatakia ushindi katika mchezo wa marudiano.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa timu ya Yanga, Andrew Ntime amesema wao kama timu wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanapata matokeo kwenye mchezo huo huku akitoa shukrani kwa Serikali kwa kuwa mstari wa mbele wakati wote wa mashindano hayo na kutoa mchango wake wa kupeleka mashabiki hao kwenye mchezo huo wa marudiano.