Faida ya nanasi kwa wajawazito

0
140

Nanasi ni tunda tamu lenye maganda ya miiba na pia linatumika kutengeza juisi.

Nanasi lina faida nyingi hasa kwa Wajawazito kutokana na kuwa na kimeng’enya cha Bromelain ambacho kinasaidia katika mtiririko wa damu kwenye mfuko wa uzazi.

Pia nanasi lina Vitamin C inayosaidia katika ukuaji wa kijusi na kupunguza kuvimba wakati wa ujauzito na kusaidia mtoto na mama kuwa salama.

Folateini iliyopo kwenye nanasi ambayo ni Vitamin B, inaelezwa kusaidia katika kutengeneza DNA na nyenzo zingine za urithi.

Kingine kilichomo kwenye nanasi ni Vitamin B6 ambayo ni muhimu katika ukuaji wa ubongo, mfumo wa Neva pamoja na mfumo wa kinga ya mwili kwa kijusi na husaidia kupunguza kichechefu kinachotokana na homa za mara kwa mara kwa Mama Mjamzito.

Nyuzinyuzi zilizomo kwenye nanasi zenyewe zinasaidia katika mmeng’enyo wa chakula na kusaidia kupata choo kwa urahisi.

Hata hivyo pamoja na
faida nyingi za nanasi hasa kwa Mama Mjamzito, haishauriwi Mama huyo Mjamzito kula nanasi kwa wingi kwa siku.

Mama Mjamzito anatakiwa asizidishe mananasi 10 kwa siku kwa sababu linasababisha kiungulia.

Wengine huamini ulaji wa nanasi unasababisha kuharibika kwa ujauzito au kujifungua kabla ya wakati. Hii haina ukweli wowote kwa kuwa bado Wanasayansi hawajathibitisha jambo hilo