Anusurika kifo kwa kutumia mvinyo na pipi

0
293

Mwanamke mmoja nchini Australia amenusurika kifo msituni baada ya kukaa huko kwa siku tano na kwa muda wote huo alikuwa akinywa mvinyo na kulamba pipi kijiti.

Kinachofanya tukio hili kuvutia zaidi ni kwamba Mwanamke huyo ni ‘teetotaller’ yaani asiyekunywa pombe kabisa.

Lillian Ip (48), alifanya safari fupi kuelekea eneo la Kaskazini Mashariki mwa Victoria Aprili 30 mwaka huu, lakini hakujua kuwa safari yake ingegeuka kuwa shida ya siku tano.

Gari lake lilikwama kwenye tope katika msitu mnene wa Mitta Mitta.

Lillian hakuweza kupiga simu kuomba msaada na familia yake ilikua na wasiwasi kwani alipokuwa hakukuwa na mawasiliano.

Kwa bahati nzuri polisi waliarifiwa na baada kumfuatilia kwa njia ya anga katika eneo la milimani, waliona gari lake.

Kwenye gari alikuwa na pipi kijiti, boksi la sharubati pamoja na chupa ya mvinyo aliyomnunulia mama yake na alianza kunywa mvinyo ilipofika siku ya tatu.

Alihofia kutopatikana akiwa hai na akiwa bado porini aliandika barua kwa familia yake iliyosema, “Ninawapenda nyote. Msinililie mimi.”