Wanawake Laki Tatu hufa wakati wa kujifungua

0
667

Takribani Wanawake Laki Tatu duniani kote, wengi wao kutoka nchi zinazoendelea wanakufa kila mwaka wakati wa kujifungua kwa njia ya upasuaji.

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Queen Mary kilichopo jijini London nchini Uingereza unaonyesha kuwa vifo vya aina hiyo katika nchi zinazoendelea viko juu tofauti na ilivyotarajiwa.

Wataalamu waliofanya utafiti huo,  wameufanya kwa Wanawake Milioni 12 kutoka maeneo mbalimbali duniani, ambao lengo la kufanya upasuaji wakati wa kujifungua lilikua ni kuokoa maisha yao pamoja na ya watoto wao.

Utafiti huo umebaini pia asilimia Kumi ya watoto wanaozaliwa duniani kote kwa njia ya upasuaji, hufariki dunia  muda mfupi baada ya kuzaliwa.

Wataalamu hao  kutoka Chuo Kikuu cha Queen Mary kilichopo jijini London nchini Uingereza wamewataka wanawake duniani kote  ambao  wanatarajia kujifungua kwa njia ya upasuaji, kutafuta hospitali zenye vifaa vya kisasa pamoja na watendaji wenye ujuzi ili kuhakikisha upasuaji huo unakua salama.