Kituo cha Mvuto kuwa mkombozi kwa wasomi

0
109

Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Waadventistista wa Sabato Kusini mwa Tanzania Mchungaji Dkt. Godwin Lekundayo amesema kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha Mvuto kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kitasaidia wanafunzi na wafanya kazi wa kituo hicho kusaidiwa kupata ufumbuzi wa mambo mbalimbali ikiwepo ajira na kujitambua.

Akizungumza kwenye harambee ya ujenzi wa kituo hicho iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Dkt. Godwin amesema Kanisa la waadventista wa Sabato limeamua kujenga kituo hicho ili kusaidia jamii ya watanzania kupata mafunzo ya kimaisha ambapo yatatolewa mafunzo ya Stadi za Maisha, Kazi za Uongozi na kuwawezesha vijana kutumia fursa ya elimu waliyoipata chuoni hapo.

Amesema kituo hicho kitakuwa kikitoa huduma mbalimbali pamoja na mafunzo ya malezi ya watoto kwa wanafunzi na watumishi wa chuo hicho.

Kituo hicho kinatarajiwa kukamilika ndani ya miaka miwili, kitagharimu Bilioni 2.5 za kitanzania ambapo kitakuwa na huduma mbalimbali za mafunzo ya kijamii.