Napoli yamaliza ukame wa miaka 33

0
303

Napoli imetwaa taji la Serie A nchini Italia kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 33, ambapo mara ya mwisho walikuwa mabingwa mwaka 1990, Hayati Diego Maradona akiwa bado ni mchezaji wa klabu hiyo.

Timu hiyo ilitoka sare ya 1-1 na Udinese baada ya Victor Osimhen kusawazisha dakika 52 ambapo walitanguliwa kwa goli la Sandi Lovric dakika 13.

Napoli imefikisha alama 80 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote, huku ikiwa bado na michezo mitano mkononi.

Hili ni taji la tatu kwa Napoli, ambapo taji la kwanza lilikuwa mwaka 1987. Hata hivyo, timu hiyo ilikumbwa na changamoto za kifedha, ikafilisika, na kushuka daraja hadi kushiriki Serie C.