Mahakama yaridhia uamuzi wa kuvuliwa Ubunge Nassari

0
532

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, – Latifa Mansour amekubaliana na uamuzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, – Job Ndugai kumvua Ubunge Joshua Nassari ambaye alikua Mbunge wa jimbo Arumeru Mashariki.

Jaji Mansour ametumia muda wa dakika 44 kusoma maelezo yake katika mahakama hiyo na kueleza kuwa Nassari alijifukuzisha mwenyewe Ubunge kwa kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge bila taarifa.

Mikutano ambayo Nassari hakuhudhuria ni wa 12, 13 na 14.

Machi 14 mwaka huu, Spika Ndugai aliiandikia barua  Tume ya Taifa ya  Uchaguzi (NEC) akieleza kuwa Nassari amepoteza sifa ya kuwa Mbunge baada ya kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo bila kutoa taarifa.