Siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani

0
127

Leo ni Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, ambapo Tanzania inaungana na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku hiyo.

Kitaifa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanafanyikia Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kwa mwaka huu yamebeba kauli mbiu inayosema ‘Kuunda Mustakabali wa Haki – Uhuru wa Kujieleza kama kichocheo cha Haki nyingine za Binadamu’.