Ala ndizi ya Milioni 281.7

0
147

Njaa imemponza mwanafunzi mmoja huko Korea Kusini ambaye amekula ndizi ambayo pengine ndiyo ndizi ghali zaidi kuwahi kuuzwa duniani na chakula cha gharama zaidi alichowahi kula.

Wakati wa maonesho ya kazi za sanaa katika onesho la WE, moja ya kazi zilizowekwa ukutani ilikuwa ni ndizi mbivu iliyoshikiliwa na gundi katika Jumba la Makumbusho la Sanaa la Leeum la Seoul ambayo ilikuwa ni kazi ya Maurizio Cattelan wa Italia.

Mwanafunzi huyo inasemekana aliichana ndizi hiyo, akaimenya na kuila bila aibu. Kisha akarudisha ganda la ndizi ukutani kwa kutumia gundi ile ile.

Makumbusho ilipomtaka aeleze ni kwa nini amefanya kitendo kile alisema kuwa, alikuwa na njaa kwani alikosa kifungua kinywa.

Ndizi hiyo iliyopewa jina la ‘Comedian’ iliuzwa kwa bei ya Dola Laki Moja na Ishirini Elfu za Kimarekani ($120,000), ambazo kwa pesa ya Kitanzania ni shilingi Milioni 281.7.