Mkurugenzi wa Mipango wa TAKUKURU mikononi mwa Polisi

0
546

Mkurugenzi wa Mipango,Ufuatiliaji na Tathmini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Kulthum Mansoor anayetuhumiwa kuwadhulumu viwanja wafanyakazi wa Taasisi hiyo amekamatwa na kufikishwa katika kituo cha Polisi cha Oysterbay kilichopo jijini Dar es salaam.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo amethibitisha kukamatwa kwa Mkurugenzi huyo na kwamba alitarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo.