Namba moja kwa vifaa vinne

0
523

Mtandao wa WhatsApp umeongeza wigo wa utoaji huduma kwa kuruhusu mtumiaji kuweza kutumia namba moja kwa vifaa vya kielekroniki vinne.

Akitoa tangazo hilo rasmi mmiliki wa mtandao huo Mark Zuckerberg amesema “Kuanzia leo, unaweza kuingia kwenye akaunti hiyo hiyo ya WhatsApp kwenye simu hadi nne.”

Kufuatia tangazo hilo mtu atakuwa na uwezo wa kupokea ujumbe kwenye vifaa vingine hata kama simu ama tarakilishi mpakato moja imezimwa kwa kutumia programu kwenye vifaa vingine.