Watu 94 kati ya 100 hatarini kuambukizwa Malaria

0
164

Watanzania wametakiwa kuendelea kujikinga na ugonjwa wa Malaria, wakati Serikali ikiendelea na juhudi za kuutokomeza kabisa ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika mkoani Dar es Salaam.

Waziri Ummy amesema kati ya watu 100, 94 wapo hatarini kupata maambukizi ya ugonjwa wa Malaria, hivyo jamii inapaswa kuongeza juhudi za kupambana na ugonjwa huo.

Amesema Wizara ya Afya itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kufuatilia ubora wa dawa za Malaria ili kujua kama zina uwezo wa kutibu ugonjwa huo au la huku lengo likiwa ni kupata mkakati wa kutokomeza kabisa ugonjwa huo.