Simba waishitaki Wydad CAF

0
829

Simba SC inatarajia kuwasilisha malalamiko yake kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) dhidi ya mashabiki wa Wydad AC kuelekea mchezo wao wa marudiano Aprili 28 nchini Morocco.

Miamba hiyo ya Tanzania inachukua hatua hiyo kufuatia tukio lililotokea katika mchezo wao wa kwanza ambapo mashabiki hao maarufu kama Ultras kuruka jukwaa na kuingia VIP B kisha wakawasha fataki zilizopelekea mashabiki na wachezaji kushindwa kuona na hivyo mwamuzi akasimamisha mchezo.

Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema malalamiko hayo yatawasilishwa CAF leo ikiwa ni tahadhari ili mashabiki hao wasiharibu saikolojia ya wachezaji wa Simba.

Simba inakwenda mjini Casablanca ikiwa na mtaji wa goli moja ililopata nyumbani, na hivyo inahitaji kupata sare au ushindi ili kufuzu hatua ya nusu fainali.