Mufti : Tunaongeza kipengele cha kulinda nchi

0
139

Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir amesema, katika mambo muhimu kwenye dini ya Kiislamu wameongeza jambo la sita ambalo ni ulinzi wa nchi.

Akitoa salamu wakati wa Baraza la Eid El Fitri Kitaifa Mufti amesema, ulinzi wa nchi ni jambo la kwanza na muhimu kwani hata viongozi wa dini watafanya kazi zao kwa amani na utulivu.

Amewataka Waumini wa dini ya Kiislamu kote nchini kulinda nchi kwa kutunza amani na utulivu, ili ustawi wa Taifa uweze kuheshimika hata nje ya nchi.

Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir pia amewasilisha salamu za Mfalme wa VI wa Morocco kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Wakati wa Baraza hilo la Eid El Fitri Kitaifa lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyererev mkoani Dar es Salaam, imefanyika ibada ya kumuombea Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.