Eid kusherehekewa kesho

0
131

Kesho ni Sikukuu ya Eid El- Fitri ambapo
Waumini wa dini ya Kiislamu nchini wanaungana na wenzao wa mataifa mbalimbali duniani kusherekea sikukuu hiyo.

Sikukuu ya Eid El- Fitri inasherekewa baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limesema,
sherehe za Eid EI-Fitri kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika mkoani Dar es Salaam.

Swala ya Eid itaswaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI, BAKWATA Makao Makuu Kinondoni kuanzia saa 1.30 asubuhi.

Swala ya Eid itafuatiwa na Baraza la Eid litakalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kuanzia saa 8.30 mchana ambqpo mgeni rasmi anatatajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.