Mbunge : Viongozi wameondolewa haki ya faragha

0
165

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) JaneJelly Ntate amesema viongozi wa Serikali wameondolewa haki yao ya faragha kwa kutokuwa na maeneo ambayo walikuwa wakiyatumia kupumzika.

Amesema kuwa Waziri hakumuondolei mtu haki nyingine za kustarehe, lakini kwa sasa hamna maeneo hayo huku akitolea mfano Leaders Club iliyopo mkoani Dar es Salaam.

“Zamani mlikuwa na faragha, mlikuwa na Leaders Club, mlikuwa na mikoani sehemu za kukaa viongozi wenyewe kwa wenyewe, kwa hiyo pale ukikaa hata ukiburudika na bia moja ukadondoka wanakubeba viongozi wenzako na hutalisikia mtaani, lakini leo hamna pa kukaa na kufanya Faragha zenu”- amesema Mbunge Ntate