Chissano: Kiswahili kimekomaa

0
162

Rais Mstaafu wa Msumbiji, Joaquim Chissano amesifu mchango wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere katika kukikuza na kukieneza Kiswahili.

Akizungumza kwa Kiswahili fasaha, akiwa ni mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Chissano ameeleza namna hotuba za Mwl. Nyerere zilivyowasaidia wengi kujifunza Kiswahili.

“Kiswahili cha Mwalimu Nyerere kilikuwa chepesi, aliweza kufikisha ujumbe kwa kila mtu hata wale wenye kujua Kiswahili cha kubabaisha,” ameeleza Chissano.

Aidha, amesisitiza matumizi ya Kiswahili katika kila nyanja kwani ni lugha yenye misamiati ya kujitosheleza na itakayoleta umoja kwa Waafrika. “Kiswahili ni lugha iliyokomaa, inaweza kutumika kwenye kila kitu.”