Bil 62.7 kukamilisha ujenzi barabara

0
136



Serikali imetoa shilingi Bilioni 62.7 kukamilisha ujenzi wa barabara ya Malagarasi – Ilunde – Uvinza, yenye urefu wa kilomita 51.1.

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Kigoma Mhandisi Ngoko Mirunge amesema, mpaka sasa ujenzi wa barabara hiyo umefikia asilimia 31.

Barabara ya Malagarasi hadi Uvinza ni sehemu ya barabara inayounganisha mikoa ya Tabora na Kigoma.

Kukamika kwa ujenzi wa barabara hiyo ya Malagarasi hadi Uvinza kupitia Ilunde, kutarahisisha usafiri na usafirishaji wa watu pamoja na bidhaa mbalimbali.