Atuhumiwa kuchanganya damu yake kwenye vinywaji

0
260

Mgahawa mmoja nchini Japan umemfukuza kazi mhudumu wake, baada ya kumshutumu kuchanganya damu yake kwenye vinywaji vya aina ya ‘cocktails’ alivyotengeneza.

Katika taarifa yake kupitia ukurasa wake wa Twitter, mgahawa huo unaojulikana kwa jina la Mondaiji uliopo katika eneo la Sapporo, Hokkaido umedai kumfukuza kazi mhudumu huyo baada ya kuwatengenezea wateja kinywaji kilichochanganywa na damu yake.

“Kitendo kama hicho hakina tofauti na ugaidi na hakikubaliki kabisa,” imesema taarifa hiyo

Mmiliki wa mgahawa huo wa
Mondaiji ambao upo katika wilaya inayofahamika kwa kuwa na starehe nyingi ya Susukino amesema, baada ya kubaini kuwepo kwa tukio hilo waliufunga mgahawa huo kwa muda wa siku moja ili kubadilisha glasi zote zinazotumiwa na wateja.

Hata hivyo uongozi wa mgahawa huo haujataja jina la mhudumu anayedaiwa kuhusika na tukio hilo la kuwatengenezea wateja kinywaji kilichochanganywa na damu yake na sababu ya mhudumu huyo kufanya hivyo.