Dkt. Mpango atoa Maagizo ‘Msafara dakika 10 zinatosha”

0
164

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango akiwa ziarani Mwanza amesema hataki kusikia tena barabara zikifungwa kwa saa nyingi ili apite, huku akisema dakika 10 zinatosha ili wananchi waendelee na shughuli zao.

Dr. Mpango amewaomba radhi wananchi kwa usumbufu walioupata baada ya Aprili 12, 2023 barabara mkoani Mwanza kufungwa kwa saa nne ili yeye apite.

“Nilishamwambia IGP na nirudie kuwaambia Makamanda wa Polisi wa Mikoa, mambo ya kufunga barabara kwa masaa mengi kisa tu mtoto wa masikini, Philip Mpango anapita, hapana.

Jana naambiwa mmefunga barabara mpaka masaa manne, haiwezekani, kwanini? Sitaki kusikia tena hili linajirudia, muambizane na wanaopokea msafara huko tutakakopita,” amesisitiza Dkt. Mpango.

Amesema “acheni wananchi wapite, kwani dakika 10 hazitoshi? Masaa manne kweli? Nawaomba radhi ya dhati kabisa Wananchi.”