Hoja ya misafara ya viongozi yaibuliwa Bungeni

0
184

Mbunge wa Viti Maalum Kunti Majala ameibua hoja ya misafara ya viongozi, ambayo amedai hutumia muda mrefu kuwasubirisha wananchi katika maeneo mbalimbali.

Kunti amesema viongozi hao wanatumia muda mrefu kuwasubirisha wananchi kuendelea na majukumu yao ilhali viongozi hao wanaweza kutumia muda mchache barabarani.

Hata hivyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama amesema, misafara hiyo ipo kwa utaratibu maalum na pia kwa usalama wa viongozi wakuu wa nchi.