Adesanya alipiza kisasi kwa Pereira

0
279

Israel Adesanya amemshinda hasimu wake Alex Pereira kwa ‘knockout’ katika mzunguko wa pili na kurejesha ubingwa wa uzito wa kati (middleweight) katika pambano la UFC 287 lililofanyika Miami nchini Marekani.

Novemba 2022 Adesanya alipoteza ubingwa huo wa uzito wa kilo 84 ambapo alikuwa ameushikilia tangu mwaka 2019 baada ya kupigwa na Pereira, raia wa Brazil, hivyo ushindi alioupata amelipiza kisasi na kurejesha mkanda wake.

Kabla ya pambano hilo, Pereira (35) hakuwahi kupigwa na Adesanya (33), ambapo kabla ya ushindi wake wa TKO na kutwaa mkanda wa ‘welter-weight’ Novemba 2022, tayari alikuwa amemshinda Adesanya mara mbili kwenye ‘kickboxing.’

“Wanasema kisasi ni kitamu,” alisema Adesanya ambaye ni mzaliwa wa Nigeria aliyekulia New Zealand, “na kwa anayenijua mimi, nina jino tamu.”