Ruvu Shooting Yazidi Kuzamishwa

0
253

Magoli matatu waliyofunga Tanzania Prisons dhidi ya Ruvu Shooting katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya umeiacha Ruvu Shooting na alama zake 20 huku wakiwa nafasi ya pili kutoka mkiani.

Ruvu Shooting ndiyo ilikuwa ya kwanza kuandika goli la mapema likifungwa dakika ya kwanza ya mchezo na Valentino Mashaka huku magoli ya wenyeji yakifungwa katika dakika ya 6 na Jumanne Elfadhili huku Jeremiah Juma akifunga magoli mawili katika dakika ya 41 na 50 ya mchezo.

Kwa matokeo hayo Tanzania Prisons inafikisha alama 28 na kusogea mpaka nafasi ya 10 kutoka ya 14 huku ikisubiri matokeo ya timu zilizo chini yake zenye uwezo wa kumshusha tena ambazo ni Mbeya City, Dodoma Jiji na Coastal Union ambazo zote zitacheza usiku huu.

Usiku huu zitapigwa mechi mbili ambapo saa 1 DODOMA JIJI itakuwa mwenyeji wa COASTAL UNION huku saa 3 NAMUNGO watawakaribisha Mbeya City katika uwanja wa Majaliwa.