Vijana msipende shortcut

0
233

Vijana nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuyafikia mafanikio ya kweli badala ya kutafuta mafanikio kwa njia za mkato.

Wito huo umetolewa mkoani Ruvuma na Askofu wa Jimbo Katoliki la Tunduru – Masasi Mhashamu Filbert Mhasi wakati wa Ibada ya Misa Takatifu ya Pasaka kitaifa katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Mtakatifu Francisco Xavery.

Katika mahubiri yake Askofu Mhasi amesema Yesu Kristo alitazama ukombozi wa Mwanadamu licha ya mateso na magumu aliyoyapitia, hatimaye kumkomboa.

“Hakuna pesa rahisi, hivyo mnapaswa kujituma katika kufanya kazi na msikubali kudanganywa kwa sababu ya fedha, kwani kwa kufanya hivyo mtaishia kupata shida na kuangamia”. amesema Askofu Mhasi

Ameongeza kuwa watu waliofanikiwa wamepitia magumu hatimaye kufikia hapo walipo, na hivyo kuwasisitiza vijana kuweka matumani yao kwa Mungu ili kupata mafanikio.