Shule ya Tanzania yaibuka mshindi wa Soka Afrika

0
326

Fountain Gate Dodoma kutoka Tanzania ndio mabingwa wa kwanza wa Mashindano ya Afrika ya Mpira wa Miguu kwa Wasichana wa Shule (CAF African Schools Football Championship).

Fountain Gate ilikuwa na wakati mwepesi kuisambaratisha Ecole Omar IBN Khatab ya Morocco kwa magoli 3-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa Afrika Kusini.

Kwa upande wa wavulana, CS Ben Sekou Sylla kutoka Guinea ndio mabingwa baada kuitoa Clapham High School ya Afrika Kusini kwa mikwaju ya penati kufuatia dakika 90 kumalizika kwa sare ya 1-1.

Kufuatia ushindi huo, kila timu itapewa dola za Kimarekani 300,000 (takribani shilingi Milioni 700).

Fainali hizo zilikuwa hitimisho la siku nne bora za soka ambapo nyota wajao wa Bara la Afrika waliweza kuonesha ubora wao.

“Tunajivunia wavulana na wasichana wote ambao wameshindana hapa, nyinyi ni kesho ya Afrika. Mataifa yenye mafanikio makubwa zaidi ya kandanda duniani huwekeza kwa vijana,” amesema Rais wa CAF, Dkt. Patrice Motsepe.