Vyura 500 wa Tanzania waishi Marekani kinyemela

0
187

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2021/2022 imebaini vyura wa Tanzania kuendelea kuishi nchini Marekani hata baada ya mkataba wa vyura hao kuwepo nchini humo kumalizika.

Vyura 500 wa Tanzania walipelekwa katika bustani za Bronx na Toledo nchini Marekani kwa lengo la kupisha ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa maji Kihansi miaka 22 iliyopita chini ya mkataba ulioisha muda wake mwaka 2020 na kuongezewa miaka miwili hadi mwaka 2022, lakini hadi leo vyura hao hawajarudishwa nchini na idadi yao ya sasa haijulikani.

Hadi sasa Serikali imetumia jumla ya shilingi Bilioni 6.69 kuwatunza vyura hao nchini Marekani.