Mashindano ya Gofu kwa vijana kufanyika Uganda

0
226

Timu ya Taifa ya Vijana ya Gofu inaendelea na mazoezi, kujiandaa na mashindano ya Afrika kwa vijana yatayofanyika Kampala, Uganda tarehe 16 hadi 21 mwezi huu.

Kocha wa timu hiyo Athuman Chiudu amesema, wachezaji wanafanya mazoezi makali na ana uhakika watafanya vizuri katika mashindano hayo.

Wachezaji wa Gofu ambao ni vijana kutoka nchi 29 Barani Afrika watashiriki katika
mashindano hayo ya Gofu kwa Vijana Barani Afrika.