Dereva apakia matofali kwenye gari la wagonjwa

0
564

Naibu Spika wa Bunge la Uganda, – Jacob Oulanyah amesema kuwa dereva aliyepakia matofali katika gari la kubeba wagonjwa atashitakiwa.

Katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twiter, -Oulanyah amesema kuwa dereva huyo amevunja sheria za utumishi wa umma kwa kutumia vibaya gari hilo.

Habari za kuwepo kwa tukio hilo la dereva wa hospitali moja ya wilaya nchini Uganda kupakia matofali katika gari la kubeba wagonjwa,  limekua likisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini humo na kuzusha hasira miongoni mwa raia wa nchi hiyo.