Sabaya kutumikia kifungo nje

0
162

Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi mkoani Kilimanjaro imemtia hatiani na kumuhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja aliyewahi kuwa nkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya baada ya kukiri makosa mawili ya kujitwalia mamlaka ambayo siyo ya kwake kisheria na kula njama ya kuzuia haki isitendeke.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi mkoani Kilimanjaro, chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Salome Mshasha imeamuru aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya aliyetiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja asijihusishe na kosa lolote la jinai wakati wa utekelezaji wa adhabu hiyo.
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi mkoani Kilimanjaro, Salome Mshasha ameamuru aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya aliyetiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja kumlipa fidia ya shilingi Milioni tano Godbless Swai kwa mkupuo mmoja.