Makundi maalum wanufaika na mabaki ya madini

0
143

Baadhi ya wanawake ambao ni wanachama wa vikundi mbalimbali wanaoshiriki mkutano unaohusisha Wachimbaji Wadogo wa Madini na Wadau wa Madini ya Viwandani unaofanyika mkoani Dar es Salaam, wameeleza namna wanavyonufaika na biashara ya kuongezea thamani bidhaa za madini.

Miongoni mwa wanawake hao ni Shamsa Diwani, Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake cha Kuongezea Thamani Madini (TAWMIWA) ambaye amesema, wamefanikiwa kukua kiuchumi kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali zitokanazo na madini.

Amezitaja bidhaa hizo kuwa ni pamoja na mapambo na urembo wa mwili na nyumba, bidhaa wanazotengeneza kwa kutumia mabaki ya madini.

Shamsa amesema mbali na kukua kiuchumi wao wenyewe, pia wanatoa mafunzo ya biashara ya kuongezea thamani bidhaa za madini na
wanufaika wa mafunzo hayo ni wanawake wastaafu, wajane, na wazazi wa watoto wenye ulemavu.