Simba milioni 50, Yanga milioni 45, fedha za ‘Goli la Mama’

0
307

Mashindano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) yamemalizika katika hatua ya makundi, huku timu za Simba na Yanga kutoka Tanzania kila moja ikifanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali katika mashindano inayoshiriki.

Wakati mashabiki wakifurahia hatua hiyo, mashabiki wa Simba pengine wana furaha zaidi kwa timu yao ndio imenufaika zaidi na ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutoa TZS milioni 5 kwa kila goli linalofungwa kwenye michezo ya kimataifa.

Simba imekusanya jumla ya shilingi milioni 50, huku Yanga ikikusanya shilingi milioni 45, lakini ahadi bado inaendelea, meza inaweza kupinduliwa au ‘gap’ likaongezwa.

CAF inatarajiwa kufanya droo ya hatua ya robo fainali leo ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho ambapo leo Simba na Yanga zitajua zinakabiliana na timu ipi.