Messi kuondoka PSG mwisho wa msimu

0
314

Klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa itaachana na utatu wa Mbappé, Messi na Neymar msimu ujao, tovuti ya RMC Sport imeripoti.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, mmoja kati ya miamba hiyo ya soka ataondoka, na kwamba anayeaminika kuondoka ni Lionel Messi, kwani klabu hiyo inalazimika kuzingatia sheria za UEFA za matumizi ya fedha.

Wakati ambapo Barcelona imeripotiwa kutaka kumsajili nyote huyo, Thiery Henry amesema ni vema mshindi huyo mara saba wa Ballon d’Or akarejea Catalan ambako aliondoka mwaka 2021.

Licha ya kufanya vizuri akiwa na PSG, Messi amekumbana na changamoto ya kuzomewa na mashabiki, hasa katika michezo miwili ya mwisho ya timu hiyo dhidi ya Rennes na Lyon.

Mashabiki hao wameripotiwa kukerwa na kitendo cha bingwa huyo wa dunia kushindwa kuisaidia timu hiyo kutwaa taji la klabu bingwa Ulaya ambapo tayari imetolewa na Bayern Munich.