Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha amesema, TBC iko tayari kushirikiana na Taasisi ya Ofisi ya Rais ya Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini
(PDB) ya Zanzibar katika kuhabarisha umma juu ya miradi mbalimbali iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Dkt. Rioba ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam, alipokutana na kufanya mazungumzo na
Afisa Mawasiliano na Habari wa PDB Mohamed Mansour, aliyetembelea ofisi za TBC zilizopo Mikocheni.
Amesema ushirikiano
kati ya TBC na PDB pia ni sehemu kudumisha Muungano, kutangaza utalii pamoja na uchumi wa Buluu.
Akiwa TBC, Mansour pia amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Huduma za Televisheni Happiness Ngasala na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Matukio, Pendael Omari.