Ataka kuvunja rekodi kwa kupika saa 97 mfululizo

0
447

Huko nchini Nigeria mfanyabiashara wa migahawa na mwandishi wa maudhui ya chakula, Hilda Baci maarufu kama Food by Hilda,  ametangaza  jaribio lake la kuvunja rekodi ya dunia ya Guinness kwa mtu mmoja kupika muda mrefu zaidi.

Ili kufanya hivyo, Hilda atatakiwa kupika kwa muda wa siku nne mfululizo, tena usiku na mchana ili apate saa 97 za kupika.

Anayeshikilia rekodi hiyo kwa sasa ni mpishi maarufu kutoka nchini India Lata Tandon,  ambaye aliweka rekodi ya kupika kwa muda wa saa 87 na dakika 46.

Hilda Baci akivunja rekodi hiyo  itamfanya kuwa mwanamke wa kwanza Barani Afrika kufikia mafanikio hayo.

Shughuli hiyo ya kupika siku nne mfululizo  imepangwa kuanza tarehe 28 mwezi huu katika bustani ya Amore huko Lagos.

Katika maisha yako muda mrefu kutumia kupika ulikuwa dakika ama saa ngapi?.