Dkt. Rioba ashiriki mkutano wa vyombo vya utangazaji

0
261

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha amesema TBC imekuwa ikifanya kazi kwa kwa uzalendo, ili kuzuia utangazaji hasi kuhusu Bara la Afrika hasa unaofanywa na vyombo vya habari vya nje ya bara hilo.

Dkt. Rioba ameyasema hayo nchini Uturuki unapofanyika mkutano wa kwanza wa vyombo vya Utangazaji vya Afrika (AUB) na vyombo vya Utangazaji vya Uturuki (TRT).

“Nchi zetu ni matajiri sana tukiamua kufanya biashara wenyewe kwa wenyewe na tukaweka agenda zetu wenyewe tutapiga hatua kwa haraka sana.” amesema Dkt.Rioba

Ameongeza kuwa hivi sasa kuna majukwaa ya mtandaoni ambayo mtu anaweza kutazama na kupata taarifa zinazoeleza Tanzania kuna nini kinaendelea, hivyo dhana ya uongo iliyoenezwa juu ya Mataifa ya Afrika inaanza kuondoka.