Stars ina mlima wa kupanda dhidi ya Uganda

0
587

Taifa Stars inatarajiwa kushuka dimbani leo nchini Misri kuikabili The Cranes (Uganda) katika mchezo wa tatu wa Kundi F wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Africa (AFCON) mwaka 2023 nchini Ivory Coast.

Stars inashuka katika Uwanja wa Suez Canal mjini Ismailia ikiwa haina rekodi nzuri dhidi ya Uganda kwani katika michezo 19, Uganda imeshinda 12, sare nne na Tanzania imeshinda mitatu.

Katika msimamo wa kundi hilo, Stars na The Cranes zimecheza michezo miwili kila mmoja, kila moja ikishinda mchezo mmoja na kupoteza mmoja, hivyo kuzifanya kila moja kuwa na alama moja.

Kwa upande wake Kocha wa Stars, Adel Ambrouche amesema licha ya maandalizi ya muda mfupi walio
yofanya, anaamini kikosi hicho kina uwezo wa kuondoka na alama tatu, wakisubiri marudiano mkoani Dar es Salaam Machi 28.

AFCON 2023 itafanyika Januari 2024 nchini Ivory Coast .