Wasio na mashamba warejeshe viuatilifu

0
194

Balozi wa zao la pamba nchini Aggrey Mwanri
amewataka
wakulima waliochukua viuatilifu na vinyunyizi vya zao hilo na ambao hawana mashamba ya pamba wavirejeshe kwenye vyama vya msingi vya wakulima katika vijiji walipovichukua.

Mwanri ameyasema hayo wakati akitoa elimu ya namna bora ya kufuata kanuni 10 za kilimo cha zao la pamba katika kata za Butinzya na
Katome halmashauri ya wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

Balozi huyo wa pamba ametaka viuatilifu na vinyunyizi hivyo kurejeshwa
baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa baadhi ya wakulima wamekuwa wakichukua viuatilifu na vinyunyizi hivyo na kutumia katika mazao mengine pamoja na katika kilimo cha bustani tofauti na ilivyokusudiwa.

Kabla ya Balozi huyo wa Pamba kwenda maeneo ya vijijini kuzungumza na Wakulima, mkuu wa wilaya ya Bukombe, Said Nkumba aliwataka maafisa ugani kwenda kwa Wakulima kutatua changamoto zao.