Kifua Kikuu (TB) huambukizwa kwa njia ya hewa na bakteria aina ya Mycobacterium tuberculosis kutoka kwa mtu mmoja ambaye auaugua ugonjwa huo kwenda kwa mwingine.
Akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC 1, Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma kutoka wizara ya Afya Dkt. Seif Mbarouk ameeleza kuwa si kila mtu aliyeambukizwa Kifua Kikuu anaugua ugonjwa huo.
“Unaweza kuambukizwa leo vimelea vya TB lakini kama kinga yako iko imara basi unaweza kuishi navyo kwa muda mrefu hata maisha yako yote bila kuugua”. amesema Dkt. Mbarouk
na kuongeza kuwa “Uwapo katika hali hii virusi hivi haviwezi kuzaliana wala huwezi kumwambukiza mtu na uhitaji matibabu”.
Kesho Machi 24, 2023 ni Siku ya Kifua Kikuu Duniani, ambapo wadau wanajadili mambo mbalimbali kuhusu Kifua Kikuu ikiwa ni pamoja mafakikio na changamoto katika mapambano ya ugonjwa huo.