Chama aingia 10 bora Afrika

0
188

Magoli matatu aliyofunga katika ushindi wa 7-0 ambao Simba SC iliupata mwishoni mwa wiki dhidi ya Horoya yamemuwezesha fundi huyo wa mpira kutoka Zambia kuwa miongoni mwa wafungaji bora Afrika.

Clatous Chama ameingia katika orodha ya wafungaji 10 bora wa muda wote katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika tangu yalipoanzishwa, akiwa na magoli 19.

Kati ya mabao hayo,15 amefunga akiwa na Simba huku mabao manne akifunga akiwa na Zesco United ya Zambia, ambapo kwa msimu huu tayari amefunga magoli matano.

Wachezaji kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote na magoli yao;

  1. Tresor Mputu : 39
  2. Mohamed Aboutrika: 31
  3. Mahmoud El Khatib: 28
  4. Flavio Amando: 27
  5. Emad Moteab: 24
  6. Ali Zitouni: 23
  7. Mbwana Samatta: 21
  8. Dioko Kaluyituka na Mouhcine Iajour: 20
  9. Clatous Chama: 19
  10. Gamal Abdel-Hamid, Kelechi Osunwa na Mudather El Tahir: 18

Katika mabao ya Chama msimu huu matatu amefunga
dhidi ya Horoya, moja dhidi ya Vipers na moja dhidi ya Primiero Agosto.