Dkt. Ndumbaro : Tanzania inaongelewa vizuri katika haki za binadamu

0
136

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amesema katika kipindi cha miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan madarakani, Tanzania inaongelewa vizuri katika haki za binadamu.

Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa hewani na TBC 1.

“Haki za binadamu ni pana, kuna haki za kisiasa, haki za kiuchumi, haki za kimazingira, sasa kwenye haki za kisiasa alichokifanya Mama ndani ya miaka miwili tunakiona. Ameruhusu mikutano ya hadhara ya kisiasa zile ni haki za binadamu.” amesema Dkt. Ndumbaro

Ameongeza kuwa ndani ya miaka miwili ya Rais Samia madarakani pia amekubali kuwepo kwa mjadala wa Katiba Mpya, haki za watu kupata elimu na haki za wasichana wanaopata ujauzito kurudi shuleni pindi wakijifungua.