Wanawake Rafiki wa Samia (Friends Of Samia) kutoka mikoa mbalimbali nchini, wamejumuika kula chakula cha pamoja katika mgahawa wa Shishi Food uliopo Dar es Salaam, ikiwa ni kuadhimisha miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan madarakani, pamoja na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Wanawake wapambanaji.
Wanawake hao wakiongozwa na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida, Martha Gwau wamesema, wanatambua kazi nzuri inayofanywa na Rais Samia na kuahidi kuendelea kumuunga mkono.
Aidha Wanawake hao wamesema sababu ya wao kukutana kwenye mgahawa wa Shishi Foos ni kuishi kwa vitendo kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan juu ya Wanawake kupendana, hivyo na wao waliamua kuonesha upendo kwa msanii Shilole kwa kula kwenye mgahawa wake.