Bikira Jane apata mtoto

0
375

Mwigizaji mashuhuri wa Marekani, Gina Rodriguez na mumewe, Joe LoCicero wamefanikiwa kupata mtoto wa kwanza miaka sita tangu wakutane kwa mara ya kwanza.

Rodriguez na mumewe walikutana wakati wa uandaaji wa tamthiliya ya Jane the Virgin 2016, walifunga ndoa 2019 na hii leo wamefanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza kiume ambaye bado jina halijawekwa wazi.

Staa huyo maarufu kama Jane Villanueva katika tamthiliya ya ‘Jane the Virgin’ (Bikira Jane) aliigiza kama binti mwenye ndoto kubwa na aliyeishia kubeba mimba na kujifungua mtoto bila kushiriki tendo la ndoa kutokana na daktari kumpandikiza mbegu alizopaswa kupandikizwa mteja mwingine na ndiyo iliyopelekea tamthilia hiyo kuitwa ‘Jane the Virgin’