Utiaji Saini ujenzi wa barabara ya Utete – Nyamwage

0
165

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila amesema, ujenzi wa barabara ya Nyamwage- Utete yenye urefu wa Kilomita 33.7 na daraja la Mbambe lenye urefu wa Mita 81 ni moja ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya Serikali.

Amesema barabara hiyo iliyopo Rufiji, Pwani, itaunganisha mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Morogoro na Tanga.

Ujenzi wa barabara hiyo ya Nyamwage – Utete utagharimu zaidi ya Dola Milioni moja za Kimarekani hadi kukamilika kwake.

Mhandisi Mativila alikuwa akizungumza mkoani Pwani wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo.