Djaro mtangazaji bora Afrika Mashariki

0
163

Mtangazaji wa TBC Fm D’jaro Arungu ameshinda Tuzo ya Mtangazaji Bora wa Redio wa Kiume wa mwaka kwa upande wa Afrika Mashariki, katika tuzo za E360 2022/2023 zilizotolewa usiku wa kuamkia leo jijini Nairobi, Kenya zikihusisha vipengele mbalimbali.

Baada ya ushindi huo, Mkurugenzi wa Huduma za Redio kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Aisha Dachi amempongeza D’jaro Arungu kwa kuendelea kuliheshimisha shirika na kulitangaza kimataifa.

“Hongera sana D’jaro kwa kushinda Tuzo ya Mtangazaji Bora wa Redio Afrika Mashariki. Hii ni furaha kubwa kwa TBC na hii ni namna bora ya kulitangaza shirika nje ya Tanzania.
Hongera, hongera, hongera sana”. amesema Dachi

D’jaro ameshinda Tuzo hiyo ikiwa miezi kadhaa imepita baada ya kushinda tuzo ya Mtangazaji Bora wa Kiume Barani Afrika katika Tuzo za ZIKOMO zilizofanyika nchini Zambia mwaka 2022.