Wasanii wampongeza Rais kwa kutoa misaada Dodoma

0
1145

Wasanii mbalimbali wamekutana wilayani Chamwino, Dodoma kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake katika miaka miwili ya uongozi wake, ambapo wametoa vifaa mbalimbali hospitalini na pilipiki kwa jeshi la polisi ili kuunga jitihada za maendeleo nchini.

Wasanii hao wakiongozwa na Ben Paul, MC Pilipili, Matonya na Dokii wamesema kuwa wamewawakilisha wenzao wengi katika kumpongeza Rais.

Wameeleza kuwa wameona maendeleo chanya katika sekta mbalimbali hivyo wao kama wasanii wameguswa kumuunga mkono Rais Samia na wanamuunga mkono kwa kasi anayoenda nayo.

Mgeni Rasmi katika makabidhiano hayo ni Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Deo Ndejembi ambaye amewashukuru wasanii hao kwa jambo jema walilolifanya kwani linamwongezea nguvu Rais katika kuendelea kuleta maendeleo nchini Tanzania.

Vifaa vilivyotolewa katika hospital hiyo ni tenki la kuhifadhi maji, sabuni, mifagio, vizoleo taka pamoja na kifaa cha kuhifadhia taka.