Balozi wa Marekani apewa zawadi ya kitabu na TBC

0
144

Balozi wa Marekani nchini Dkt. Michael Battle amepewa zawadi ya kitabu cha “The Roadmap to Success For President Samia Suluhu Hassan” na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha.

Kitabu hicho kinazungumzia uongozi na mafanikio ya Rais Samia Suluhu Hassan, tangu aingie madarakani.

Balozi huyo wa Marekani nchini amepewa zawadi hiyo leo Machi 10, 2023, alipotembelea ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania zilizopo Mikocheni, Dar es Salaam kwa lengo la kujionea shughuli za uendeshaji, kufahamu historia ya TBC pamoja na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Dkt. Ayub Rioba Chacha.