Mbowe : Wabunge 19 viti maalum hatuwatambui

0
106

“Kitendo cha kupeleka Wabunge 19 ambao hawakutokana na maamuzi yetu ndani ya chama ni uvunjaji wa Katiba, ni uvunjaji wa maadili na kitendo hicho ni uhuni ambao hauwezi kuvumiliwa na mtu yeyote”.

“Taasisi kama Bunge ambayo inapaswa kutunga sheria lakini inashiriki katika haya, pamoja na kuwa Spika anafahamu hakuna zuio lolote la wao kuwepo ndani ya Bunge lakini wameendelea kuwepo humo”.

“Wale wanajiwakilisha wao wenyewe na familia zao hawamwakilishi mtu yeyote mule bungeni”

“Mheshimiwa Rais with due respect (kwa heshima kubwa) nakuomba uhurumie zile kodi za Wananchi ambazo mnawalipa wale Wabunge na hawamwakilishi mtu yeyote mule.”